Latest News
TANGAZO KWA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI OMAN KUHUSU PASIPOTI MPYA ZA AFRIKA MASHARIKI:
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN UNAPENDA KUWATAARIFU WATANZANIA WANAOISHI NCHINI OMAN KUWA UTARATIBU WA KUTOA PASIPOTI MPYA ZA AFRIKA MASHARIKI HAUJAANZA KUFANYIKA HAPA UBALOZINI. KWA WAKATI HUU TUNAWAOMBA MUENDELEE KUVUTA SUBIRA WAKATI SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA INAENDELEA KUKAMILISHA MAANDALIZI YA KUFUNGA VITENDEA KAZI VYA KUWEZESHA OFISI ZAKE ZA KIBALOZI KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA PASIPOTI MPYA ZA AFRIKA YA MASHARIKI. AIDHA, UBALOZI UNAENDELEA KUPOKEA FOMU ZA MAOMBI YA PASIPOTI ZINAZOTUMIKA SASA AMBAZO MWISHO WAKE WA MATUMIZI UTAKUWA MWAKA 2020. VILE VILE, KWA SASA INASHAURIWA KUWA KILA ANAYEPATA NAFASI YA KUSAFIRI KWENDA TANZANIA, AKAOMBE KUBADILISHIWA PASIPOTI AKIWA TANZANIA.

 

KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI WASILIANA NASI AU FIKA UBALOZINI

 

TUNAWATAKIA KAZI NJEMA

 

IMETOLEWA TAREHE: 21/11/2018